Afisa wa NIDA hatiani kwa ubadhirifu wa dola 8,779 za safari za kikazi kwa watumishi

DAR-Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Bw.Humphrey Einhrad Haule amefikishwa mahakamani na kufunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba ECC. 28546/2024.
Oktoba 4, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kupitia shauri hilo,Mshtakiwa Humphrey akiwa Afisa Usajili chini ya Kitengo cha Utawala na Fedha pamoja na majukumu mengine alipangiwa majukumu ya kushughulikia safari za kikazi kwa watumishi wa NIDA.

Akitekeleza jukumu hilo, inadaiwa alifanya ubadhirifu wa fedha za safari za viongozi wa NIDA na kuzitumia kwa manufaa yake binafsi na hivyo anashtakiwa kwa makosa ya kufanya ubadhirifu wa dola za kimarekani 8,779.

Ni kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022 na kosa la wizi kwa mtumishi wa umma kifungu 270 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022 .

Aidha, shauri tajwa limesomwa mahakamani hapo na mshtakiwa amekana makosa yote na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo kupelekwa Rumande.

Kesi hii imesomwa na waendesha mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Kinondoni, Wakili Aidan Samali na Thuwaiba Hussein mbele ya Mhe. Ramadhan Lugemalira, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani Oktoba 22,2024 kwa ajili ya kusomwa hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news