Ajali ya basi yaua na kujeruhi 36

MWANZA-Watu nane wamefariki dunia na wengine 36 wamejeruhiwa baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Nyehunge kugongana na basi la Asante Rabi.
Ni katika ajali iliyotokea alfajiri ya saa 12 Oktoba 22,2024 katika eneo la Ukiriguru Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo chake ni mwendokasi.

Amesema, ajali hiyo imetokea baada ya basi la Asante Rabi lenye namba za usajili T458 DYD lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Arusha kujaribu kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari na hivyo kuligonga basi la Nyehunge.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news