Ajali ya lori la mafuta yaua 11 Uganda

KAMPALA-Jeshi la Polisi mjini Kigogwa nchini Uganda limesema, watu 11 wakiwemo watoto wawili wamekufa baada ya lori la mafuta kupata ajali na kulipuka nchini humo.
(Picha na Badru Katumba / AFP).

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Jeshi la Polisi limesema ajali hiyo ilitokea saa tisa alasiri Oktoba 22,2024 katika mji wa Kigogwa takribani kilomita 25 Kaskazini mwa mji mkuu wa Kampala.

Wamebainisha kuwa, baadhi ya miili iliharibiwa na moto huku ikishindwa kutambulika na majengo manne yakiteketezwa na moto huo.

Lori hilo lilikuwa likisafiri kutoka Kampala kwenda Gulu Kaskazini mwa Uganda, ambayo ni safari ya takribani kilomita 650 hadi kufika huko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news