Akiba Commercial Bank Plc yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja

DAR-Akiba Commercial Bank Plc imewashukuru wateja wake kwa kuungana nao katika safari hii ya kutoa huduma bora zaidi za kibenki ambazo zinachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania.
Shukrani hizo zimetolewa leo Oktoba 9,2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Hafla iliyofanyika katija tawi la Ubungo la benki hiyo na kuhudhuriwa na wateja, wafanyakazi wa benki na wawakilishi wa vyombo vya habari.
Mkurugenzi huyo amesema, wiki ya huduma kwa wateja wameifanya kwa namna ya kipekee kwa kutambua thamani ya wateja kwa kutoa tunzo,kwani kufanya hivyo ni kuonesha ahadi ya benki ya kuendelea kutoa huduma bora.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Above and Beyond” ikimaanisha kwenda zaidi ya matarajio, kauli ambayo inakusudia kuhamasisha utoaji wa huduma bora zaidi kwa wateja.
“Niwashukuru wateja wetu kutuchagua kuwa washirika wenu wa kibiashara kwani bila nyinyi, tusingeweza kufikia mafanikio haya tunayojivunia leo hivyo wiki hii ni maalum kwa ajili yenu, tunathamini na kutambua mchango wenu,”amesema Arumasi.

Hata hivyo Akiba Commercial Bank Plc imefanya maboresho yaliyofanyika katika huduma za kidijitali za benki, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ACB Mobile na Akiba Wakala kwa kuzingatia mahitaji ya wateja.

Pia,ina huduma mpya ya Internet Banking inayopatikana kwa wateja binafsi, makampuni makubwa na taasisi mbalimbali, kama sehemu ya mkakati wa mabadiliko ya kidijitali wa benki hiyo kwa kauli mbiu “Twende Kidijitali.”“Kwa kuzingatia mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia.

"Mwaka 2024 tumeamua kuupa jina la Mwaka wa Kidijitali,’ na tumejidhatiti kuwafikishia huduma za kibenki kwa njia ya kisasa zaidi kupitia mifumo yetu ya kidijitali,” aliongeza Bw. Arumasi.

Maadhimisho ya wiki hii, Akiba Commercial Bank inafanya shughuli mbalimbali katika matawi yake yaliyopo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya, na Dodoma ili kuwapa wateja fursa ya kuona na kushiriki katika maboresho yanayoendelea kufanywa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw.Silvest Arumasi akitoa hati ya shukrani kwa Bi. Twaiba Msechu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi la Ubungo.

Aidha,benki itaendelea kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja ili kuboresha bidhaa na huduma zake kwa ujumla.“Wiki hii siyo tu kwa ajili ya sherehe, bali ni ahadi yetu ya kuendelea kuboresha na kutoa huduma bora ambazo zitazidi matarajio yenu,” amesema Bw. Arumasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news