KINSHASA-Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mheshimiwa Said Mshana amekutana na kuzungumza na Waziri wa Michezo na Burudani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Didier Budimbu Ntubuanga.
Kikao hicho kimefanyika ofisini kwa Mhe. Waziri Ntubuanga jijini Kinshasa.


Taifa Stars inakutana na Timu ya Taifa ya DRC maarufu kwa jina la Chui, kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kufanyika nchini Morroco mwaka 2025.