Balozi Naimi awasilisha hati za utambulisho IAEA

VIENNA-Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mashirika ya Umoja wa Mataifa jijini Vienna nchini Austria, Mheshimiwa Naimi Aziz amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Mhe. Rafael Mariano Grossi katika tukio lililofanyika tarehe 10 Oktoba, 2024.
Wakizungumza baada ya tukio la kukabidhi Hati, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na IAEA kwenye matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa ajili ya maendeleo ya sekta mbalimbali nchini hususan afya, kilimo na usalama wa chakula, afya, ufugaji na nishati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news