Balozi wa India nchini Tanzania atembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

DODOMA-Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Balozi Bishwadip Dey, tarehe 3 Oktoba, 2024 amefanya ziara ya kutembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyoko Mtumba jijini Dodoma, ambapo lengo kubwa la ziara hiyo ni kujitambulisha na kufanya mazungumzo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu masuala nambalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mhe. Balozi wa India, kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwandishi Mkuu wa Sheria Bw. Onorius Njole amemshukuru Mhe. Balozi kwa kuitembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku akiwa na matumaini kuwa ziara hiyo itabainisha fursa mbalimbali ambazo zitendeleza ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Nchi ya India.
“Mhe Balozi tunakukaribisha sana kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, natumaini kupitia ziara hii Ofisi yetu itaweza kufahamu masuala mbalimbali ya kisheria yanavyotekelezwa India, pia ni fursa nzuri ya kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizi mbili,”amesema Mwandishi Mkuu wa Sheria.
Kwa upande wake Balozi wa India Nchini Tanzania Mhe. Balozi Bishwadip Dey ameshukuru na kufurahishwa kwa mapokezi aliyoyapota katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kuelezea fursa mbalimbali za kisheria zilizopo nchini India ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo, ikiwemo mafunzo mbalimbali ya Uandishi wa Sheria, Uaandaji wa Maamuzi ya Mahakama na Usuluhishi wa Migogoro nje ya Mahakama.

Aidha, Mhe. Balozi amezungumzia suala la matumizi ya teknolojia ya Akili Mnemba katika utekelezaji wa majukumu ya kisheria, ambapo amesema ipo haja ya Tanzania kujifunza matumizi ya akili mnemba ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kisheria.
“Teknolojia imekuwa kwa kasi kwenye masuala mbalimbali Imani yangu kupitia ziara hii utakuwa mwanzo mzuri wa wataalamu hususani wa sheria kutoka Tanzania watapata fursa nzuri ya kujifunza matumizi ya teknolojia katika kuendesha shughuli za kisheria hivyo kurahisisha utendaji kazi wao,"amesema Mhe. Balozi Bishwadip.

Ziara hiyo ya Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Balozi Bishwadip Dey kutembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mwendelezo wa kuimarisha ushirikiano ulipo kati Tanzania na India pamoja na uhusiano wa kidiplomasia kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news