Barabara ya lami kilomita 7.7 yenye thamani ya shilingi bilioni 9.3 kuunganisha mikoa ya Singida,Simiyu na Arusha

SINGIDA-Wakazi wa Wilaya ya Iramba na Mkalama mkoani Singida, wanatarajia kunufaika na barabara ya kiwango cha lami inayojengwa kuunganisha mikoa ya Singida, Simiyu, hadi Arusha. Mradi huu, wenye thamani ya shilingi bilioni tisa, umefikia asilimia 65 ya utekelezaji.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, ametembelea na kukagua mradi huo ambao ukikamilika utawasaidia wananchi katika usafirishaji wa mazao ya kilimo, hivyo kuimarisha biashara.
Amesema,ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo unaoonesha namna Serikali inavyofanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake bila ubabaishaji.
Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Singida, Msama Msama alieleza kuwa, kipande cha barabara kinachojengwa kati ya Kitukutu-Gumanga-Mkalama na Chemchem-Sibiti, kikiwemo Kitukutu-Kinampanda, chenye urefu wa kilomita 7.7, kitagharimu bilioni 9.31 na kinajengwa na mkandarasi mzawa.

“RAIS SAMIA NA MAENDELEO, WASIKIE NA WAONE”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news