Benki ya Dunia yakagua miradi ya maji Pangani,yaridhika

TANGA-Wataalamu wa Wizara ya Maji na wawakilishi wa Benki ya Dunia wamekagua mradi wa maji wa Sange na Zahanati ya Masaika wilayani Pangani na kuridhishwa na utekelezaji wake.
Kazi hiyo inafanyika mkoani Tanga ikiwa ni ufuatiliaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira iliyotekelezwa kupitia fedha za Progamu ya Lipa kwa Matokeo (PforR) katika Sekta ya Maji.
Mradi wa maji Sange una thamani ya shillingi milioni 540 na umeanza kuhudumia wananchi ambapo utekelezaji wake ni asilimia 90.

Ujenzi wa mradi huo umehusisha tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 5000,ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukuma maji na ujenzi wa vituo vya umma vya kuchotea maji 13 na ulazaji wa mabomba zaidi ya Mita 9,900.
Kwa usafi wa mazingira katika Zahanati ya Masaika kazi imehusisha ujenzi wa kichomea taka,eneo la kitakasa mikono,ujenzi wa vyoo vya watumishi na matundu ya vyoo kwa huduma ya wagonjwa ,ujenzi wa mnara na ununuzi wa tanki la kuhifadhia maji.
Wilaya ya Pangani kwa sasa hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama imefika asilimia 92 na wananchi wameshukuru serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kufanikisha huduma ya maji kwa watu wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news