Bonanza la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani Mkalama lafana

SINGIDA-Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka wananachi wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Mpiga Kura ili wawe na sifa za kuchagua viongozi katika Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.Wito huo ameutoa Oktoba 6,2024 wakati wa Bonanza la Hamasa ya Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa lililofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Nduguti inayopatikana katika Kata ya Nduguti wilayani Mkalama.
“Ili uweze kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 unapaswa kuwa umejiandikisha katika Daftari la orodha ya Wapiga Kura. Hivyo wenye Umri kuanzia miaka 18, nawasihii mjitokeze kujiandikisha ili muwe na sifa ya kuchagua viongozi mnaowataka,” Mhe. Machali.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amesema kuwa zoezi la uandikishaji Orodha ya Wapiga Kura litaanza tarehe 11-20, Oktoba 2024 na zoezi hilo litachukua muda wa siku 10 hivyo wananchi watumie fursa hiyo kujitokeza kwa wingi.
“Kama unataka kumchagua kiongozi umpendae hakikisha unajiandikisha,” amesema Mhe. Machali.

Kwa upande wake, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Wilaya, Bwana Mohamed Atiki ametoa rai kwa vijana na wanawake wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
“Vijana wenye umri kuanzia miaka 21 na kuendelea, pamoja na kina mama nawasihi mjitokeze kwa wingi mgombee nafasi za uongozi ili kwa pamoja muwe sehemu ya mabadiliko katika jamii zetu lakini pia wananchi wenye sifa wakati wenu ni huu wa kuchagua viongozi mnaowataka,” amesisitiza Atiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news