BoT na TRA wazikutanisha benki, taasisi za fedha kujadili Hati ya Uwakala katika ulipaji wa kodi nchini

DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda wamekutana na Wakuu wa Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kujadili suala la Hati ya Uwakala katika Ulipaji wa Kodi nchini (Agency Notice).
Gavana wa Benki Kuu Bw. Tutuba akifungua kikao hicho, amesema lengo la kukutana pamoja kati ya Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mabenki na Taasisi za Fedha ni kuona namna wanavyoweza kuboresha utendaji wa kazi kwa kushirikiana na kuweka mazingira rafiki ya biashara kwa wananchi bila vikwazo vyovyote.
Gavana Tutuba amesema Benki Kuu ya Tanzania itahakikisha inasimamia vyema Taasisi za Fedha na kutatua changamoto zilizopo ili wanaotakiwa kulipa kodi walipe bila kushurutishwa kama Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoagiza.
Akizungumza katika Kikao hicho kilichofanyika Benki Kuu ya Tanzania, Kamishna Mkuu Mwenda amesema kuwa Hati za Uwakala ni njia ya mwisho kabisa ya kukusanya kodi na TRA itaendelea kutoa elimu na kujenga mahusiano ya karibu zaidi na walipakodi ili waweze kulipa kodi zao kwa wakati kwa lengo la kuondokana na matumizi ya Hati hizo za uwakala katika Ulipaji wa Kodi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news