BoT:Taarifa kwa umma kuhusu kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ya Tanzania

DAR-Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kuanza kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000), na elfu kumi (10000) za matoleo ya mwaka 1985 hadi 2003, pamoja na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010. Hii ni kufuatia Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.
Katika taarifa iliyotolewa Oktoba 26, 2024 na Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel M. Tutuba, zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza Januari 6, 2025 hadi Aprili 5, 2025. Badiliko hili litafanyika kupitia ofisi zote za Benki Kuu na benki za biashara, ambapo wananchi watapewa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa.

Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia kufanya malipo popote duniani. Vilevile, benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.

Kufuatia zoezi hilo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilichotolewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news