CCM itashinda kwa kishindo 2025,tujitokeze kujiandikisha katika daftari-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema, CCM ina kila sababu ya kushinda uchaguzi ujao wa 2025 kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho 2020 -2025 iliyovuka malengo katika sekta mbalimbali za maendeleo.Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 22, 2024 alipozungumza katika kongamano maalum Jumuiya ya Wazazi Tanzania la kupongeza juhudi za miaka minne ya uongozi wake na Serikali anayoiongoza ya awamu ya nane kwa maendeleo na mafanikio makubwa yaliyopatikana hapa nchini, lililofanyika viwanja vya Verde Marina, Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha,Rais Dkt. Mwinyi ameiagiza Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanyakazi ya uhamasishaji kuhakikisha Wanachama wa chama hicho wenye sifa wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwakani Januari.

Alifahamisha, kwa kufanya hivyo CCM, itakuwa na uhakika wa kupata wingi wa kura na ushindi mkubwa usio na mashaka na kuondosha malalamiko ya wapinzani kila wanaposhindwa uchaguzi.

Halikadhalika Dkt.Mwinyi amewasisitiza wanachama na viongozi wa jumuiya zote za Chama hicho kuendelea kujipanga vema na kufanyakazi za chama kwaajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Vilevile Dkt. Mwinyi amepongeza uamuzi wa Jumuiya ya Wazazi kuandaa Kongamano maalum la kumpongeza kwa mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake, na kuongeza kuwa hatua hiyo imemuongezea ari na motisha yeye na watendaji Serikalini ya kufanya mambo makubwa zaidi kuwaletea wananchi maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news