JOHANNESBURG-Aliyekuwa kocha wa Young African Sports Club, Cedric Kaze raia wa Burundi ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Kaze anatarajiwa kufanya kazi chini ya Mtunisia, Nasreddine Nabi ambaye pia alifanya naye kazi Young Africans Sports Club (Yanga SC) ya jijini Dar es Salaam.
“Ongezejo hili la kimkakati kwenye timu yetu ya ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi linalenga kuimarisha utendaji wa klabu na matarajio ya msimu huu."