CGP Katungu ateta na uongozi wa SHIMA

DODOMA-Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Jeremiah Katungu, Oktoba 03, 2024 amekutana na Watendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Magereza (SHIMA) kwaajili kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji wa shirika hilo ili liweze kuleta tija zaidi katika uzalishaji.
SHIMA lilianzishwa mwaka 1983 kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika Namba 23 ya mwaka 1974 (The Corporations Sole {Establishment} Act CAP119 R.E. 2002) pamoja na kanuni zake za Mwaka 1983 (The Corporation Sole {Prisons Department} Regulations GN 128 of 1983. Na marekebisho yake ya GN 179 ya 1983, GN 640 ya 1986 na GN 155 ya 2001.
Shirika hilo ni chombo ndani ya Jeshi la Magereza kinachofanya shughuli za uzalishaji kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1974. Tofauti na mashirika mengine ya umma shirika hilo linaendesha shughuli zake kiuchumi kwa njia ya kuzungusha mtaji wake wa ndani kufanya biashara.
Vilevile, shirika hilo lina jukumu la kurekebisha wafungwa (Urekebu) kupitia shughuli zinazofanyika kwenye miradi kwa kutoa stadi za kazi na ujuzi utakaowezesha kumbadilisha tabia baada ya kutumikia kifungo.
SHIMA linafanya kazi zake za uzalishaji kibiashara ili kusaidia Serikali katika kuhudumia mahitaji ya kuendesha shughuli za Jeshi la Magereza kupitia faida itakayozalishwa na Shirika na kuchangia pato la Serikali ktpitia kodi na tozo mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news