Chukia Hali ya Sasa:Mbwa ni wararuaji, nguruwe wachafuaji

NA LWAGA MWAMBANDE

TUNAAMBIWA kwamba CHUKIA HALI YA SASA, yaani tuchukie hali tuliyonayo kwa lengo la kufanya bidii ili hali zetu ziwe bora zaidi. Kwamba tuachane na kawaida, tufanye mambo mapya.
Baadhi ya mashairi yaliyo katika Diwani hii ni pamoja na Maisha ya kawaida, Usiwe wa kawaida, Toka kwenye chimbo lako, Ewe mwanamwali wewe, na Acha huo unguruwe:
SOMA:Hufungua Yangomoyo

Mbwa ni wararuaji, nguruwe wachafuaji,
Akishapata kilaji, kwa hicho chako kipaji, _
Sasa hawakuhitaji, kumbwa na shida hawaji,
Wape lulu wakanyaga, mema wanayapuuza.

Aidha, kuna mashairi ambayo yanawaasa watumishi wa Mungu, kutumika kwa kuiga mfano wa Bwana Yesu ambaye alitumika mijini na vijijini:

Hebu tuvae viatu, na kotekote tufike,
Huko tuwakute watu, Neno la Mungu lifike,
Mambo yote yenye kutu, kotekote yatoweke,
Yesu alifanya kazi, mijini na vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news