Dereva wa TPA na wenzake saba mahakamani kwa kusababisha hasara ya shilingi bilioni 26 za mafuta

DAR-Tino Ndekela ambaye ni dereva wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na wenzake saba wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 20.
Miongoni mwa mashtaka hayo ni utakatishaji wa zaidi ya shilingi bilioni 20 na kuisababishia Kampuni ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER) Tanzania hasara ya shilingi bilioni 26.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanakabiliwa na mashta nane ya wizi wa zaidi ya Lita Milioni 6.3 za mafuta ya diesel, na mashtaka nane ya wizi wa zaidi ya lita milioni 3.5 za wa mafuta aina ya Petrol mali ya Tiper.

Mashtaka mengine yanayowakabili washtakiwa ni uharibifu wa wa mali kwa lengo la kutoa huduma ya zaida, Utakatishaji na shtaka moja la kuisababishia Tiper hasara.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Cathebert Mbilingi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki, imewataja washtakiwa wengine kuwa ni Fikiri Kidevu, Amani Yamba, Mselem Abdallah Kika Sanguti, Twaha Salum, Audience Shayo, Hamis Hamis

Akisoma hati ya mashtaka, Mbilingi amedai kuwa kati ya Januari 2019 na Desemba 2022 huko Tungi katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, washitakiwa waliaribu miundombinu ya bomba la kusafirishia mafuta ya Disel na Petrol Mali ya Tiper.

Katika kosa la wizi inadaiwa siku na mahali hapo katika nyakati tofauti, washtakiwa wote waliiba mafuta hayo ya Diesel na Petrol mali ya Tiper.

Imeendelea kudaiwa kuwa, kati ya January Mosi na Desemba 2022 huku Tungi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, washtakiwa kwa makusudi waliisababishia Tiper hasara ya Sh. 26,019,047,803.99.

Wakili Mbilingi amedai kuwa, kipindi hicho hicho katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, washtakiwa walijipatia kiasi cha Sh. 20,huki wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Aidha,washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa DPP.

Hata hivyo,kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Novemba 4,2024 na washtakiwa wote wamerudishwa rumande hadi siku tajwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news