Dkt.Mataragio aongoza kikao cha maandalizi Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika jijini Cape Town

CAPE TOWN-Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio leo Oktoba 6, 2024 ameongoza kikao cha maandalizi cha Wataalam kutoka Tanzania watakaoshiriki Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week). Kikao kimefanyika jijini Cape Town nchini Afrika Kusini.
Kongamano hilo litafanyika kuanzia tarehe 07 hadi 10, Oktoba, 2024 nchini humo.
Maudhui ya kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news