WASHINGTON D.C-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameshiriki mjadala kuhusu kuiwezesha Afrika kuwa na nishati ya uhakika, ulioandaliwa na Taasisi ya Mission 300, Kando ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia jijini Washington D.C nchini Marekani, na kuzihimiza nchi za Afrika kwa kushirikiana na Taasisi za Fedha Duniani pamoja na Sekta Binafsi, kuhakikisha kuwa zinawekeza kwenye uzalishaji wa nishati ya uhakika na yenye gharama nafuu ili kutimiza malengo ya kujiimarisha kiuchumi, kuchochea uwekezaji, uzalishaji wa bidhaa na huduma na kukuza ajira.