MANYARA-Ķatibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameridhishwa na hatua ya urejeshwaji wa hali katika makazi mapya ya waathirika wa maafa yaliyotokea Wilaya ya Hanang mwishoni mwa mwaka 2023, yaliyosababishwa na maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka mlima Hanang na kusababisha vifo, upotevu wa mali, makazi ya wananchi pamoja na uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja ya mita ya maji katika nyumba zilizojengwa kwa ajili ya waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka mlima Hanang’ zilizojengwa katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Warret katika Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.
Ameyasema hayo mara baada ya ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya mradi wa nyumba 108, za waathirika wa maafa hayo katika eneo la Gidagamowd lililopo katika kitongoji cha Warret katika wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’,Mhe.Almishi Issa Hazali wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa nyumba 108 za waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka mlima Hanang zilizojengwa katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Warret katika Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.
Dkt. Yonazi ameoneshwa kuridhishwa na hatua iliyofikiwa na kueleza kuwa, mradi utakabidhiwa kwa wakati kama ilivyokusudiwa ili kuhakikisha hali inarejea kama ilivyokuwa awali, na kuendelea na shughuli za uzalishaji na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
“...nitumie fursa hii kuwapongeza kwa jitihada mnazoendelea nazo katika urejeshaji hali, niendelee kusisitiza kuwa, muendelee kuchukua jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kuzuia na kupunguza madhara ya majanga na kujiandaa na kukabiliana na maafa nchini,” alisema Dkt. Yonazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka mlima Hanang’ zilizojengwa katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Warret katika Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe.Almishi Issa Hazali.
Mhandisi kutoka TANROADS, Erinest Mbuya akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi na Timu aliyoongozana nayo kuhusu mradi wa nyumba za waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka mlima Hanang’ zilizojengwa katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Warret katika Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.
Muonekano wa baadhi ya nyumba za waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka mlima Hanang’ zilizojengwa katika eneo la Gidagamowd lililopo katika Kitongoji cha Warret katika Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ na Mwenyekiti wa Kamati Elekezi ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya Mheshimiwa Almishi Issa Hazali ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha jamii inaendelea kupata elimu zaidi juu ya masuala ya maafa, na kuishukuru Serikali kwa namna inavyojali wananchi katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na wanaendelea kujiletea maendeleo yao.
“Tumefarijika ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Yonazi, tunaendelea kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa zinazotekelezwa na kuendelea kutenga fedha kuhakikisha masuala ya menejimenti ya maafa yanaratibiwa vyema kwa upande wa Hanang tutaendelea kutoa ushirikiano kwa wanachi na wadau mbalimbali katika kuhakikisha suala la maafa linakabiliwa kama ilinavyoelekezwa,” alisema Mhe. Almishi.