Falsafa za Baba wa Taifa zinatekelezwa kwa vitendo nchini-Rais Dkt.Mwinyi

MWANZA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa, kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu imeonesha umuhimu kwa Taifa linalohitaji maendeleo, sambamba na kuwa na mazingira endelevu yatakayochangia maendeleo ya nchi.
Amefafanua kuwa, ni jambo jema kuona miaka 25 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, falsafa zake zinaendelea kuishi na kutekelezwa kwa vitendo, huku akiwahimiza Watanzania kuziendeleza.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 14, 2024 alipozungumza katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukizi ya miaka 25 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Rais Dkt. Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusimamia malengo ya viongozi waasisi wa Muungano, ambayo yanaendelea kuwaunganisha Watanzania.

Halikadhalika, Dkt. Mwinyi amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarisha na kuunga mkono Muungano kwa mshikamano wa Watanzania.
Rais Dkt. Mwinyi amewasisitiza wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wananchi kwa maandalizi mazuri ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, kumbukumbu ya Baba wa Taifa, na Wiki ya Vijana Kitaifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news