Hakuna sababu za kuihofia Akili Mnemba (AI)-Yusuph Kileo

NA GODFREY NNKO

WATANZANIA wameshauriwa kutoogopa matumizi ya Akili Mnemba (AI) kwa kuhofia inakuja kupoka kazi zao na badala yake waitumie kama fursa kwa sababu imekuja kutoa fursa nyingine mpya za ajira.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni katika Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA Tanzania lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) na Yusuph Kileo ambaye ni Mtaalam wa Masuala ya Usalama wa Mtandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidigitali.

"AI,imekuja kuzalisha ajira nyingine nyingi kwa sababu AI kama AI, teknolojia hii ili iweze kufanya kazi inahitaji wahandisi.

"Wahandisi ambao watatusaidia kufanya hizo coding, kuifanya vile ilivyo kwa sababu haiwezi yenyewe kujitengeneza.

"Lakini itahitaji wale watu wanaohusika na mambo ya data...data entry na kadhalika kwa ajili ya kuiongezea ama kuipatia taarifa kama hizo data.

"Lakini, vile vile itahitaji watu wenye hiyo elimu ya sensor au elimu ya kutengeneza hizo components, hizo zote ni ajira mpya zitakuja kuzaliwa.

"Lakini, inazalisha ajira nyingine nyingi sana kutoka vyanzo tofauti tofauti vingi, kwa hiyo, hiyo dhana kwamba AI itakuwa na changamoto kwenye upande wa ajira.

"Ninafikiri si suala ambalo tunapaswa sana kulipa uzito kwa sababu pia kuna postive impact katika kutengeneza ajira nyingine nyingi."

Kileo anasema,tunachopaswa kukifanya ni sisi tuikumbatie mara moja na tuwe wabunifu ili kuweza kuinua hizo fursa pale pale zinazokuja na hii teknolojia ya AI.

"Na kuachana na zile dhana hasi ambazo zipo ambapo kwenye kila kitu pia kina faida pamoja na hasara yake.

"Pia,tuongeze nguvu kufikiria kwenye mazuri yake na tuikumbatie maana yake ipo na haitakimbia kokote, inaendelea kukuwa na itaendelea kubadilika.

"Tuongezee watu wetu uwezo ili kuweza kui-adopt vizuri tukaenda nayo katika speed ambayo wanayo ili kuweza kupata manufaa yake kwetu na kusahau upande wa madhara.

"Kwa sababu ni ukweli usiopingika kwamba kupitia hii AI, sasa hivi masuala haya ya customer relations ndiyo kitu kikubwa ambacho tumekiona sasa hivi kama faida, kwamba unaweza ukapiga simu inapokelewa huko, mtu hayupo, lakini inaendelea kuongea na inaweza kukujibu kadri unavyobonyeza namba ya uhitaji kulingana na maelekezo ya kupata hizo huduma."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news