Huduma za uchunguzi wa magonjwa sasa kupatikana wilayani Mwanga

KILIMANJARO-Wananchi wa Halmashauri ya Wilya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro sasa wanasogezewa huduma za afya za uchunguzi wa magonjwa ikiwemo huduma za upimaji wa kansa ya matiti kwa akina mama pamoja na Ultrasound kwa ajili ya kina mama wajawazito.
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo leo Oktoba 7, 2024 alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga unaotekelezwa kwa fedha za Serikali ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Kilimanjaro.

"Kwa sasa mgonjwa akitakiwa kupata huduma za X-Ray anakwenda Hospitali ya Mawezi au KCMC ambapo ni urefi wa Kilometa zaidi ya 50, lakini kwa sasa huduma hizo zitapatika katika Wilaya ya Mwanga zilizoletwa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Huduma hizi zitasaidia kuokoa gharama za wananchi wetu wa Mwanga kwenda kutunza mgonjwa wao mbali, zitasaidia kuokoa uchumi wetu maana mtu badala ya kuwaza mambo ya kuongeza uchumi atawaza mgonjwa yupo KCMC, Rais wetu amesema hapana inatosha, hayo yote yafanyike wapi? Hapahapa Mwanga," amesema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amesema, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni Mbili za mradi wa ujenzi wa Hositali hiyo ya Wilaya ya Mwanga pamoja na Milioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali hiyo.
Amesema, miongoni mwa vifaa vitakavyo nunuliwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na mashine ya kupima kansa ya matiti kwa akina mama, Ultrasound kwa ajili ya kina mama wajawazito pamoja na dawa ambao ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Nimeingia pale kwenye jengo la mionzi, nimekuta digital X-Ray ambayo ni toleo la kisasa kabisa, inauwezo wa kugeuza mwili wa mgonjwa pamoja na kupiga picha kwa ajili ya uchunguzi, haya mlikua mnayaona wapi ndugu zangu?.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha inatoa tiba sahihi kwa wakati sahihi, kwa mahitaji sahihi kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga,"amesisitiza Waziri Mhagama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news