Hufungua Yagomayo:Jitahidi pata kitu, ili uongezwe kitu

NA LWAGA MWAMBANDE

HUFUNGUA YAGOMAYO, hii ni diwani inayomwelezea huyu ambaye kwake hakuna lisilowezekana.

Yeye anaweza yote hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu yanaonekana kwamba hayawezekani.
Utapata mashairi ya kukutia moyo, kukutoa mahali pamoja na kukufikisha mahali bora zaidi katika imani yako kwa Mungu aliye hai.

Ni mashairi ambayo yametungwa kwa kuzingatia Neno la Mungu. Kwa mfano:

...Naenda si nguvu zangu, zile za watu wa Mungu,
Wanaomuomba Mungu, kwa haya maisha yangu,
Anawasikia Mungu, aleta kupona kwangu,
Vinginevyo ningegota, kwa kushindwa kusafiri.

Na lingine linasema:

...Kama ukiwa na kitu, Mungu huongeza kitu,
Endapo hauna kitu, usitarajie kitu,
Jitahidi pata kitu, ili uongezwe kitu,
Kwa kujipatia kitu, unazivuta baraka.

Hivyo, utapata pia fursa ya kufanya rejea katika Biblia na kuzidi kujifunza zaidi na kuimarisha imani yako.

Yanafaa kusoma, kuimba na kutumia hata unapokuwa na faragha na Mungu wako: Karibu ubarikiwe na diwani hii ya HUFUNGUA YAGOMAYO. Bofya,soma kurasa zote hapa>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news