WASHINGTON D.C-Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeimwagia sifa Tanzania kwa namna inavyosimamia sera zake za uchumi na fedha ikiwemo kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.

Kiongozi huyo amesema kuwa nchi nyingine za Afrika zinalo la kujifunza kuhusu usimamizi wa uchumi na sera za fedha kutoka Tanzania kutokana na umahili wake katika eneo hilo ambapo nchi imekuwa imara kiuchumi licha ya misukosuko mingi ya kiuchumi na kijamii inayojitokeza duniani.