Jaji Mkuu wa Tanzania kushiriki mkutano wa kujadili Mamlaka ya Kikatiba Afrika

NA MARY GWERA
Mahakama Harare

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 30 Oktoba, 2024 amewasili Mjini Victoria Falls nchini Zimbabwe kuhudhuria Mkutano wa saba wa Mamlaka ya Kikatiba Afrika (CJCA) unaotarajia kufanyika kuanzia kesho tarehe 31 Oktoba, 2024 hadi tarehe 03 Novemba, 2024.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya wageni waliowasili leo nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa saba wa Mamlaka ya Kikatiba Afrika (CJCA).

Mhe. Prof. Juma ataungana na Majaji na Wadau wengine wa Sekta ya Sheria kutoka nchi mbalimbali kushiriki Mkutano huo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika chumba cha wageni maalum (VIP) wakati alipowasili leo tarehe 30 Oktoba, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Victoria Falls nchini Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa saba wa Mamlaka ya Kikatiba Afrika (CJCA).

Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo; Utu wa binadamu kama thamani ya msingi na kanuni: Chanzo cha tafsiri ya kikatiba, ulinzi wa haki za msingi za binadamu na utekelezaji.

Aidha, katika Mkutano huo, Mhe. Prof. Juma atakuwa kwenye moja ya Paneli ya Wazungumzaji watakaozungumzia na kuongoza majadiliano kuhusu mada isemayo; Dhana ya utu wa binadamu katika sheria ya kikatiba.
Wageni wengine kutoka nchini mbalimbali wakiwa wamewasili nchini Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo.
Kibao maalum kwa ajili ya kukaribisha wajumbe wa Mkutano wa saba wa Mamlaka ya Kikatiba Afrika (CJCA).
Wenyeji wakiendelea na taratibu za kupokea wageni waliofika leo tarehe 30 Oktoba, 2024 kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa saba wa Mamlaka ya Kikatiba Afrika (CJCA).
Sehemu ya Maafisa walioambatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.
Wageni wakipanda moja ya mabasi kwa ajili ya kuwapeleka katika maeneo waliyofikia.(Picha na MARY GWERA, Mahakama ya Tanzania).

Aidha, Mkutano huo utahudhuriwa pia na Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman.

Mbali na Tanzania, nchi nyingine zitakazoshiriki katika Mkutano huo ni Zambia, Malawi, Msumbiji, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia, Somalia, Sierra Leone, Togo, Uturuki, Misri, Ushelisheli, Urusi, Senegal na nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news