MWANZA-Mratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Bi. Numpe Mwambenja ameikumbusha jamii kuendelea kulinda mazingira ili kuepuka uwezekano wa kukumbwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu.
Mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Numpe Mwambenja akizungumza wakati wa semina kuhusu ya masuala ya menejimenti ya maafa kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Ameyasema hayo wakati akifungua semina kuhusu ya masuala ya menejimenti ya maafa kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza katika kuelekea Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa Dunia Oktoba 13, 2024.
Kitaifa mwaka huu yanaadhimishwa mkoani Mwanza yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ni Msingi katika Kulinda na Kuwawezesha Vijana kwa Mustakabali wa Baadae usio na Maafa.”
Kwa upande wake Mratibu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Maendeleo kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid Bw. Tema Hassan amesema masuala ya kukabiliana na maafa yanahitaji elimu mahususi huku akisisitiza matumizi ya teknolojia ya kisasa ili kuifikia jamii iliyokusudiwa.
“Teknolojia ni muhimu katika kuifikia jamii kiurahisi , hivyo ni vyema kuwekeza katika matumizi ya simu na mifumo ya kisasa kwa kuzingatia makundi yanayokusudiwa,” amesema Temu.
Mratibu wa Maafa Dawati la AFYA MOJA Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Mwanaisha Mrisho akiwasilisha mada kuhusu njia bora za kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu wakati semina kuhusu ya masuala ya menejimenti ya maafa kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kufuatia hatua hiyo Bw.Temu amesema kuwa Shirika la ActioAid litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukabiliana na maafa nchini kwa kuzingatia unyeti wa masuala hayo na kuhakikisha jamii inaendelea kuwa stahimilivu katika masuala ya maafa.
Mratibu wa Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Maendeleo kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la ActionAid, Bw. Tema Hassan akieleza mchango wa shirika hilo katika masuala ya menejimenti ya maafa wakati wa semina kuhusu masuala ya maafa kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Kwa upande wake Afisa Afya wa Kata ya Kirumba, Bi. Veronica Massawe amesema usafi wa mazingira ni jambo lisiloepukika huku akiitaka jamii kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu ili kujikinga na magonjwa ya milipuko.
“Ni muhimu kulinda afya zetu kwani, Afya ndiyo mtaji wetu sote," amesisitiza Bi. Veronica Massawe.
Afisa Afya Kata ya Kirumba, Bi. Veronica Massawe akizungumza wakati wa semina kuhusu ya masuala ya menejimenti ya maafa kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
"Tumejiandaa, kukabiliana na maafa ikiwa na pamoja na kujiepusha na mazingira hatarishi yanayoweza kutuletea maafa katika kata yetu, usafi ni wajibu wa msingi kuwa na vyoo bora na kuvitumia katika kupambana na magonjwa ya mlipuko."
Naye Mwenyekiti wa Wahudumu wa Afya ya Jamii Kata ya Kirumba Bw. Wilfred Roman amesema watatumjia elimu waliyopewa katika semina hiyo kwa kuwaelimisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa kufanya afya shirikishi.
Mhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kata ya Kirumba Bi. Mary Mary Mpanduji akichangia jambo wakati wa semina kuhusu ya masuala ya menejimenti ya maafa kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHW) katika Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
“Elimu tuliyopewa katika semina ni nyenzo muhimu tutakayoitumia katika kupambana na magonjwa ya mlipuko,”amesema Wilfred.