Kayuni atembelea banda la BoT maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa

MBEYA-Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Emmanuel Kayuni, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, kuanzia tarehe 21 hadi 26 Oktoba 2024.
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” yanatoa fursa kwa wananchi kujifunza kuhusu usimamizi wa fedha binafsi; uwekaji wa akiba; mikopo; uwekezaji katika dhamana za serikali; watoa huduma za fedha; usimamizi wa sekta ya fedha; mifumo ya malipo na namna BoT inawalinda watumiaji wa huduma za fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news