Kikosi cha Mbwa na Farasi chazindua kampeni ya tuwaambie kabla hawajaharibiwa

DAR-Kikosi cha Mbwa na Farasi Makao Makuu ya Kikosi hicho kilichopo jijini Dar es Salaam wamezindua Kampeni ya Tuwaambie kabla Hawajaharibiwa, lengo likiwa ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuongea na watoto kabla hawajapata changamoto za ukatili.
Akiongea mara baada ya matembezi hayo maalum yaliyolenga kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, Mkuu wa Kikosi hicho nchini Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Namsemba Mwakatobe amesema, Jeshi la Polisi limeanzisha kampeni hiyo maaalum lengo likiwa nikuliokoa kundi hilo ambalo katika siku za hivi karibuni limeonekana kuwa katika changamoto ya Ukatili.
Ameongeza kuwa, wananchi wanayo nafasi ya kupaza sauti na kuwaambia watoto juu ya vitendo vya ukatili na kuwakumbusha kuyasema mapito na changamoto wanazopitia.
Sambamba nayo amebainisha kuwa kampeni hiyo ni mahususi kwa ajili ya kuwakumbusha wananchi hususani wazazi na walezi kuongea na watoto juu ya madhara ya ukatili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news