🔴LIVE:Waziri Mkuu mgeni rasmi hafla ya kufunga Kongamano la Nane la Mwaka la TEHAMA Tanzania 2024

Leo Oktoba 17,2024 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kufunga Kongamano la Nane la Mwaka la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Tanzania.

Kongamano hili ambalo lilianza Oktoba 13,2024 katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam lilifunguliwa Oktoba 15,2024 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb).

Aidha,kongamano hili limeongozwa na kauli mbiu isemayo Kutumia Uwezo wa Akili Mnemba na Roboti kwa Mapinduzi ya Kiuchumi na Kijamii. Kauli mbiu hiyo inafungua mjadala muhimu hususani kwa wakati huu ambapo Dunia nzima inashuhudia mapinduzi ya kidigitali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news