FARIDA RAMADHANI
NA JOSEPH MAHUMI
VIONGOZI wa kimila (Machifu) jijini Mbeya wameiomba Serikali kuweka programu ya elimu ya fedha kuwa endelevu ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata uelewa na kutatua changamoto mbalimbali za masuala ya kifedha.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (Kulia), akiwakaribisha Machifu wa Jiji la Mbeya walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Wametoa wito huo walipotembelea Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwa mwaka 2024 yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe Jijini Mbeya, yaliyobeba kauli mbiu ya “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (Kulia), akitoa maelezo kuhusu Maadimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwa Machifu wa Jiji la Mbeya, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, wakati wa Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Akizungumza kwa niaba ya Machifu hai, Chifu Lyoto, alisema elimu ya fedha ni muhimu kwa kuwa inatoa mwongozo wa namna bora ya kutumia fedha, umuhimu wa uwekaji akiba, mikopo pamoja na namna bora ya kujikwamua kiuchumi.
Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyanza, akitoa elimu ya Fedha kwa Machifu na wawakilishi wa vikundi vya kijamii jijini Mbeya, kuhusu utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kuweka akiba pamoja na kupanga bajeti walipotembelea Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta Maadhimisho haya Mbeya, tunaiomba iendelee kutuletea hii elimu hasa katika maeneo ya vijijini kwa kuwa masuala ya fedha ni muhimu katika maisha yetu,”alisema Chifu Lyoto.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Emmanuel Kayuni (kushoto), akimsikiliza kwa makini Afisa Tehama Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bi. Zaina Mwanga, kuhusu Mfumo wa Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali (GePG), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Alisema katika Maadhimisho hayo wamejifunza mengi kuhusu masuala ya fedha na watatumia elimu hiyo kuwaelimisha wengine ambao hawajapata nafasi ya kufika katika viwanja hivyo.
Aidha, aliwakaribisha wananchi wote wa jiji la Mbeya na viunga vyake kutembelea Maadhimisho hayo ili kupata elimu muhimu kwa maendeleo yao na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Emmanuel Kayuni (kushoto), akimsikiliza Mhasibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Kurthum Juma, kusuhu masuala ya madeni, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-razaq Badru, akiagana na Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Mudith Cheyo baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Mtunza Kumbukumbu kutoka Kitengo cha Pensheni, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally, akimkabidhi kipeperushi kinachoelezea aina ya mafao yanayotolewa na Wizara ya Fedha, mmoja wa wananchi wa jiji la Mbeya, waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mbeya, Bw. Marco Fihavango, akitoa elimu kuhusu mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) tawi la Mbeya, walipohudhuria madarasa yanayoendelea katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 ambao pamoja na mambo mengine elimu kwa umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa Mpango huo.
Machifu wa jiji la Mbeya wakiongozwa na Chifu Lyoto wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayoendela katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka jijini Mbeya na mikoa jirani.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Mbeya).
Maadhimisho hayo yanalenga kuelimisha wananchi kuhusu matumizi ya huduma rasmi za fedha pamoja na kuongeza mchango wa Sekta ya Fedha kwenye ukuaji wa Uchumi.