GENEVA-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 149 wa IPU uliofanyika jijini Geneva nchini Uswisi amewataka Wajumbe wa Bunge hilo kumuamini na kumpa nafasi afanye kazi yake na waache kufikiria dhana ya Ukoloni kwa wanaofikiria hivyo ikiwemo kupinga kila kitu kwa kuwa anatokea Tanzania au Afrika. Dkt.Tulia ameyasema hayo baada ya baadhi ya wajumbe kukosoa uamuzi wake wa kufanya ziara nchini Urusi na kukutana na Rais Vladimir Putin kuhusu vita ya Ukraine badala ya kwenda Gaza ambapo,Dkt.Tulia amesema alipochaguliwa tu Novemba, mwaka jana alienda Israel na Palestine na kuonana na viongozi na kusema hajachagua upande kwenye migogoro yote na kwamba IPU inapambana kurejesha amani kwenye migogoro hiyo.
“Mimi sio Mungu, sio Malaika, ni Binadamu, nafanya kilicho ndani ya uwezo wangu, kikosi kazi kiliniambia nifanye nilichofanya kosa langu ni nini."
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo