KAGERA-Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemtambulisha kwa Wananchi na kumkabidhi eneo la mradi Mkandarasi Kampuni ya Shandong Luqiao Group atakayeanza ujenzi wa barabara ya Kyerwa – Omurushaka (km 50) kwa kiwango cha lami na kuuagiza Wakala ya Barabara (TANROADS) kumsimamia Mkandarasi huyo ili barabara hiyo ikamilike kwa wakati bila ya kusuasua.
Hafla ya kumkabidhi Mkandarasi imefanyika Oktoba 18, 2024 katika eneo la Rwenkorongo Wilayani Kyerwa ambapo Bashungwa ameeleza ujenzi wa barabara utaziunganisha Wilaya za Karagwe na Kyerwa kwa kugharamiwa na Serikali kwa Shilingi Bilioni 94.34.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo