DAR-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema jumla ya watanzania 31,282,331 wamejiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, ambao ni sawa na asilimia 94.83 ya lengo la kuandikisha wapiga kura 32,987,579.