Mawakili wa Serikali wanolewa kuhusu upekuzi wa mikataba

DODOMA-Divisheni ya Mikataba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendesha mafunzo ya Upekuzi wa Mikataba kwa Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, mafunzo hayo yanafanyika kwa siku tano jijini Dodoma, kuanzia leo Oktoba 7 hadi 11 Oktoba, 2024.
Akizungumzia mafunzo hayo Wakili wa Serikali Mwandimizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Ildefonce Mkandala amesema mafunzo hayo kwa Mawakili wa Serikali yanalenga kuwaongezea uwezo na kubadilishana uzoefu kati ya Mawakili hao, ili waweze kuboresha utekelezaji wa majukumu yao husasani katika eneo la upekuzi wa mikataba na utoaji ushauri kwenye mikataba ambayo Serikali au Taasisi zake inakusudia kuingia. Aidha, Wakili wa Serikali Mwandamizi amesema kuwa mafunzo hayo yanaambata na uwasilishwaji wa mada mbalimbali ambazo zimejikita zaidi katika maeneo ya Upekuzi wa Mikabata mbalimbali, namna ya utoaji wa ushauri kwenye mikataba ambayo Serikali inakusudia kuingia, pia masuala yanayohusua ya Mikataba ya Kimataifa.
“Tumewapitisha kwenye maeneo muhimu ambayo Wakili wa Serikali anapaswa ayazingatie wakati anapofanya upekuzi wa mikataba na kutoa ushauri juu ya mikataba mbalimbali na tunaamini baada ya mafunzo haya watakuwa wamepata ujuzi wa kutosha utakaoboresha utendaji kazi wao,”amesema Wakili wa Serikali Mwandamizi.

Kwa upande Wakili wa Serikali,Bi. Irene Msuya ameishukuru na kuipongeza Divisheni ya Mikataba kwa kuandaa mafunzo hayo, kwakua kupitia elimu wanayoipata kwenye mafunzo hayo itawasaidia katika kuongeza ufanisi kwenye shughuli zinazohusiana na mikataba.
“Mafunzo haya ni muhimu kwetu katika kufanikisha shughuli zetu tunazozifanya wakati wa kuikagua mikataba mbalimbali, kutoa ushauri na kushughulikia mikataba ya kimataifa, pia tunatagemea baada ya mafunzo haya ufanisi wetu katika utendaji kazi utaongezeka,”amesema Wakili wa Serikali,Bi. Irene.
Mafunzo ya Upekuzi wa Mikataba kwa Mawakili yanayondeshwa na Divisheni ya Mikataba ni Mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na Divisheni katika kuwajengea na kuwaongezea ujuzi Mawakili wa Serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news