GABORONE-Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM),Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na Mabalozi kutoka nchi za SADC wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana katika kikao kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 21 Oktoba 2024.

Ameeleza kuwa, amekutana nao ikiwa ni sehemu ya ratiba zake mbalimbali ili kuwasiliana nao moja kwa moja na hivyo kusaidia waangalizi kupata picha halisi ya jinsi maandalizi ya uchaguzi huo kwa ujumla yanavyokwenda.
Amesema, SEOM imejipanga na iko tayari kutekeleza jukumu lake la Uangalizi kwa ukamilifu kama walivyoaminiwa na Jumuiya na kuwatuma kuifanya kwa niaba yao.
Amesema, wao kama viongozi wa SEOM watakuwa na mikutano na watu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusikiliza na kupata maoni ili kuhakikisha kazi yao ya uangalizi inakwenda vizuri.
