■Ateta na Watumishi nchi nzima
■Asisitiza weledi katika kuwahudumia Wananchi
DODOMA-Maboresho makubwa ya TEHAMA yanayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kwenye mifumo yake ya utoaji wa huduma, yanakwenda kuondoa changamoto nyingi zilizokuwa zikisababishwa na makosa ya kibinadamu na kuwawezesha wanachama kujihudumia wenyewe bila ya kufika ofisini.
Akizungumza na Watumishi wa Mfuko wa Kada ya Ofisa Udhibiti Ubora, Madai na Uanachama, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka ameweka wazi kuwa maboresho ya mifumo yanayoendelea kufanyika yanakwenda kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama na wadau wake wote hivyo kuongeza imani na kuridhika kwa wadau.



Akizungumzia mafunzo kwa maofisa hao, Dkt. Isaka amesema kuwa ni fursa nzuri kwa watumishi kujikumbusha miongozo mbalimbali, maadili ya utumishi, kubadilishana uzoefu na kupata taarifa mpya katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Baada ya mafunzo haya ambayo yamelenga maeneo ya Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, Mwongozo wa Uandikishaji Wanachama, Matekelezo na mabadiliko ya miongozo mbalimbali mtaweza sasa kuwahudumia wateja wetu vizuri na kwa wakati,” amesema Dkt. Isaka.
Amesema, katika kipindi hiki cha kuelekea utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, Mfuko umefanya maandalizi ya kutosha katika kuwahudumia wananchi wengi zaidi ili lengo la Serikali liweze kufikiwa na wanachi wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote.
...‘Bima ya Afya kwa Wote, jiunge sasa’...
Tags
Afya
Dr Irene Isaka
Habari
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
NHIF Tanzania
Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote