Mifumo ya taasisi saba yaanza kusomana

DAR-Katika mwaka 2023/24, Kituo cha Uwekezaji kimekamilisha ujenzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuhudumia Wawekezaji (Tanzania Electronic Investment Window - TeIW) kwa awamu ya kwanza ambao ulizinduliwa Septemba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan. (PICHA NA MAKTABA).

Mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya Taasisi saba (7) ambazo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Kazi, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na TIC.

Mfumo huo, unamuwezesha mwekezaji kusajili mradi popote ndani na nje ya nchi na kupata vibali vya uwekezaji ndani ya siku 3 ikiwa ametimiza vigezo.

Awamu ya pili ya ujenzi wa mfumo huo itahusisha uunganishaji wa Taasisi nyingine saba (7) ambazo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Kilimo, Tume ya Madini na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news