Minziro ndiye Kocha Mkuu mpya Pamba Jiji FC

NA DIRAMAKINI

PAMBA Jiji FC imethibitisha kumteua kocha Fred Felix 'Minziro' kuwa Kocha Mkuu akichukua mikoba ya Goran Kopunovic aliyetupiwa virago Oktoba 16, 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 17, 2024 na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Ezekiel Ntibikeha akibainisha kuwa, Minziro atashirikiana na Kocha msaidizi Mathias Wandiba.

“Uongozi wa Klabu ya Pamba Jiiji Fc, unautaarifu umma kuwa umeingia makubaliano na kocha Fred Felix ‘Minziro’ kuwa Kocha Mkuu akichukua mikoba ya Goran Kopunovic,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, kwa uteuzi huo wana Mwanza wana matumaini kuiona Pamba Jiji ikifanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pamba Jiji FC inashika nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 4 baada ya michezo 7, haijashinda mechi yoyote, imetoka sare 4 na kupoteza 3.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news