Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji yazinduliwa rasmi

MAPUTO-Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume amezindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi leo tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliowashirikisha wadau mbalimbali muhimu wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Msumbiji, Wawakilishi kutoka Serikali ya Msumbiji, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, Jumuiya za Kiraia na waandishi wa habari, Mhe. Dkt. Karume ameishukuru Serikali ya Msumbiji kwa kuialika Misheni hiyo ambayo ina jukumu la kuangalia namna misingi ya demokrasia, taratibu na kanuni za uchaguzi za SADC zinavyotekelezwa.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizindua rasmi Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi tarehe 03 Oktoba 2024 katika hafla iliyofanyika jijini Maputo. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.

Amesema,Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC pamoja na mambo mengine itatathmini mwenendo wa uchaguzi kulingana na Kanuni na Miongozo ya SADC inayoongoza Uchaguzi wa Kidemokrasia iliyorekebishwa mwaka 2021 na kuridhiwa na nchi wanachama.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na na Waangalizi 52 wa SADC kwa lengo la kuwaaga kabla ya kusambazwa katika majimbo 11 ya uchaguzi nchini Msumbiji kwa ajili ya kuangalia uchaguzi. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini Msumbiji unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.

Amesema pamoja na mambo mengine, Kanuni na Miongozo hiyo inazitaka nchi wanachama kushirikisha wananchi katika mchakato wa demokrasia, kuwawezesha wananchi kufurahia haki za binadamu na kuwa huru katika kushirikiana, kukusanyika na kujieleza.

Kadhalika kanuni na miongozo hiyo imeweka mikakati ya kuzuia rushwa, upendeleo, migogoro ya kisiasa, kutovumiliana na kuhakikisha zinakuwepo fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa katika kutumia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Serikali na kuhakikisha uhuru wa wananchi kupata taarifa kuhusu masuala ya uchaguzi unazingatiwa.
Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama , Prof. Kula Ishmael Theletsane akizungumza wakati wa uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Mjumbe wa Troika ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Phaustine Kasike akishiriki hala ya uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Mjumbe wa Troika ambaye pia ni Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema akishiriki hafla ya uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.

Mhe. Dkt. Karume pia alitumia fursa hiyo kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na Misheni ya Ulinzi wa Amani ya SADC nchini Msumbiji (SAMIM), ambayo ilifanikiwa kudhibiti vikundi vya kigaidi vilivyoibka katika maeneo ya Kaskazini mwa Msumbiji na kuishukuru Serikali ya Msumbiji kwa kuahidi kuendelea kulinda mafanikio yaliyofikiwa na SAMIM katika eneo hilo.

Vilevile, Mhe. Dkt. Karume alilipongeza Jeshi la Ulinzi la Msumbiji na vyombo vingine vya Usalama vya nchi hiyo kwa jitihada zao zilizofanikisha Wananchi katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo wanajiandikisha kwa ajii ya kupiga kura licha ya changamoto za kiusalama.
Mjumbe wa Troika ambaye ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri akifuatilia uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Sehemu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Sehemu nyingine ya waangalizi.
Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC nchini Msumbiji wakishiriki uzinduzi wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC nchini Msumbiji. Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge nchini humo unatarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.

Mhe. Dkt. Karume alitumia nafasi hiyo pia kuwatakia uchaguzi wa amani na utulivu wananchi wa Msumbiji na kutoa wito kwa wale wote waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 09 Oktoba 2024 na kupiga kura. Pia alitoa rai kwa wadau wote wa siasa nchini Msumbiji kuheshimu maoni na mitazamo tofauti ya kisiasa miongoni mwao na kujua wajibu wao katika kipindi chote cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Naye Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Prof. Kula Ishmael Theletsane alieleza umuhimu wa Misheni za Uangalizi kuwa zinalenga kufikia malengo mahsusi ya mafanikio hususan kwa mtangamano wa SADC kupitia kanuni ya ustahimilivu, utekelezaji wa demokrasia, utwala bora na amani.

Misheni ya SADC, iliwasili nchini Msumbiji tarehe 24 Septemba, 2024 na itakuwepo nchini humo hadi tarehe 20 Oktoba, 2024 kwa lengo la kuangalia uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni na Miongozo ya SADC inayoongoza Uchaguzi wa Kidemokrasia iliyorekebishwa mwaka 2021.
Sehemu nyingine ya waangalizi wa uchaguzi.
Meza kuu katika picha ya pamoja.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Msumbiji walioshiriki hafla ya uzinduzi wa misheni hiyo.
Picha ya pamoja ya kundi la waangalizi wa uchaguzi.
Picha ya pamoja ya waangalizi wa uchaguzi.
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi.

Misheni hiyo ya SADC ina jumala ya wajumbe 97 ambapo miongoni mwao 52 ni waangalizi wa uchaguzi ambao watasambazwa kwenye majimbo 11 ya uchaguzi nchini Msumbiji ambayo ni Cabo Delgado, Nampula, Niassa, Maputo City, Maputo, Tete, Gaza, Inhambane, Sofala, Manica na Zambezia.

Waangalizi hao wanatoka katika Nchi 10 ambazo ni wanachama wa SADC. Nchi hizo ni Tanzania, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Eswatini, Malawi, Namibia, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news