MAPUTO-Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume tarehe 06 Oktoba 2024 ameongoza kikao kazi cha Wakuu wa Misheni za Kimataifa za Uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akiongoza kikao kazi cha Wakuu wa Misheni za Kimataifa za Uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024. Kikao hicho kilifanyika tarehe 06 Oktoba, 2024 jijini Maputo na kuhudhuriwa na Wakuu wa Misheni za Uangalizi kutoka Umoja wa Afrika (AU-EOM), Mhe. Bornito de Sousa Baltazar Diogo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Angola, Umoja wa Ulaya (EU-EOM), Jumuiya ya Madola, Mhe. Kenny Anthony, Waziri Mkuu Mstaafu wa Saint Lucia na Jaji Dkt. Manuel Pereira da Silva wa Jukwaa la Uchaguzi la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (ECF-SADC).
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Msumbiji kutoka Umoja wa Afrika (AU-EOM), Mhe. Bornito de Sousa Baltazar Diogo, Makamu wa Rais Mstaafu wa Angola akishiriki kikao cha Wakuu wa Misheni za Ungalizi za Kimataifa kilichoongozwa na Mhe. Dkt. Karume.
Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji kutoka Jukwaa la Uchaguzi la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (ECF-SADC), Mhe. Jaji Dkt. Manuel Pereira da Silva akishiriki kikao cha Wakuu wa Misheni za Ungalizi za Kimataifa kilichoongozwa na Mhe. Dkt. Karume.
Mhe. Dkt. Karume akisalimiana na Mhe. Kenny Anthony, Waziri Mkuu Mstaafu wa Saint Lucia ambaye pia ni Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji kutoka Jumuiya ya Madola.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Wakuu wa Misheni za Uangalizi kutoka Umoja wa Afrika (AU-EOM), Umoja wa Ulaya (EU-EOM), Jumuiya ya Madola na Jukwaa la Uchaguzi la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (ECF-SADC).
Misheni ya uangalizi ya Umoja wa Afrika inaongozwa na Makamu wa Rais Mstaafu wa Angola, Mhe. Bornito de Sousa Baltazar Diogo huku Misheni ya Jumuiya ya Madola ikiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Saint Lucia, Mhe. Kenny Anthony.
Mhe. Dkt. Karume akiteta jambo na Mhe. Kenny Anthony, Waziri Mkuu Mstaafu wa Saint Lucia ambaye pia ni Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji kutoka Jumuiya ya Madola.
Mhe. Dkt. Karume akizungumza na Mwakilishi wa Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya Umoja wa Ulaya. Kushoto ni Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa.
Balozi Mussa akisalimiana na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Msumbiji kutoka Umoja wa Afrika (AU-EOM) na Makamu wa Rais Mstaafu wa Angola, Mhe. Bornito de Sousa Baltazar Diogo.
Picha ya pamoja ya Wakuu wa Misheni za Uangalizi za Kimataifa.
Picha ya pamoja ya Wakuu wa Misheni za Kimataifa za Uangalizi wa Uchaguzi nchini Msumbiji wakiwa na Wajumbe wa Troika kutoka Tanzania ambao ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ay Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mussa (kushoto) na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema (kulia).
Picha ya pamoja.
Aidha, Misheni ya Umoja wa Ulaya inaongozwa na Mbunge katika Bunge la Ulaya, Mhe. Laura Ballarin Cereza na Misheni ya ECF-SADC inaongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Angola, Jaji Dkt. Manuel Pereira da Silva.