Mo Simba Arena mbioni kujengwa

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Simba Sports Club, Mohammed Dewji amesema kuwa, kwa sasa kinachosubiriwa ndani ya klabu hiyo ni mchakato wa mabadiliko ili ujenzi wa Mo Simba Arena uanze.
Mo Dewji ambaye pia ni mwekezaji katika klabu hiyo ya jijini Dar es Salaam ameyasema hayo leo Oktoba 6,2024 katika Mkutano Mkuu wa Mwaka 2024 wa Klabu ya Simba.

"Hii ni ramani mpya ya Mo Simba Arena. Mradi mkubwa ambao utaweka msingi wa mafanikio yetu baadae.

"Tunatarajia kujenga kambi bora ya mazoezi itakuwa na gym, majengo ya malazi, kituo cha lishe, bwala la kuogolea, kituo cha burudani.

"Viwanja vitano vya kisasa zaidi ya hayo kujenga makumbusho ya klabu na kuanzisha chuo cha maendeleo ya vijana ili kulea vipaji vya soka nchini.
“Ili kufanikisha yote haya tunasubiri mchakato wa mabadiliko ya Simba kukamilika, tuko katika hatua za mwisho, ujenzi wa miundombinu hii unakuja na gharama kubwa, ni ngumu kuanza huu ujenzi bila mfumo kubadilika,”amesisitiza Mo Dewji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news