DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. William Lukuvi amesema, ujenzi unaoendelea wa tenki kubwa la kuhifadhia maji safi kutoka Ruvu unatarajia kukamilika mapema mwakani ambapo litasaidia kuondoa kero ya maji jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe.William Lukuvi akikagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi tenki la maji Bangulo lililopo Pugu Stesheni jijini Dar es Salaam.
Waziri ametoa kauli hiyo Oktoba 10,2024 alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi na kuzungumza na wananchi wa Bangulo katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa,ujenzi wa bwawa hilo utanufaisha wananchi takribani 450,000 hasa wa Jimbo la Ukonga na Segerea na Mkandarasi ameshalipwa fedha zote, hivyo mradi utakapokamilika wananchi wote wataunganishwa na mtandao wa maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe.William Lukuvi akikagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi tenki la maji Bangulo lililopo Pugu Stesheni jijini Dar es Salaam.
“Hivyo tutashuhudia kata saba katika Jimbo la Ukonga zitakazoondokana na adha ya upatikanaji wa maji.
"Aidha,tunashuhudia fedha nyingi zinatolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji na barabara na tumekubaliana usanishaji wa mikataba ufanyike katika maeneo husika ya ujenzi wa miradi."
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe.William Lukuvi akiwa pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azan Zungu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Tukuyu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. William Lukuvi akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila wakikagua Barabara ya Tukuyu mara baada ya kuzindua.
"Ujenzi wa miradi ya maendeleo ni hatua, lakini sisi tumekwenda kasi sana katika utekelezaji wake, hivyo wananchi mkiona vinaelea vimeundwa."
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Albert Chalamila amesema,Mkoa umejikita sana katika kulinda amani na kuendelea kulinda raia na mali zao, ili wananchi waweze kujikita katika shughuli za uzalishaji.
“Mwenyeviti wa Serikali za Mitaa na kamati za ulinzi kwa kushirikiana na polisi jamiii, hakikisheni madhila ya wananchi kuogopa wahalifu yanadhibitiwa katika maeneo yenu,“ alisema Mkuu wa Mkoa Chalamila.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo amesema, Serikali imejenga madarasa ya ghorofa zaidi ya 80 na madarasa ya kawaida 465 kwa shule za sekondari, na kwa upande wa shule za msingi madarasa zaidi ya 437 yamejengwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe William Lukuvi akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Robert Chalamila wakipata maelezo ya mchoro wa mradi wa ujenzi wa tenki la maji Bangulo lililopo Pugu Stesheni jijini Dar es Salaam.
“Mafanikio haya yanakuja kutokana na mahusiano tuliyonayao na wawakilishi wa wananchi wanaochagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya miradi ya maendeleo,” alisema Mkuu wa Wilaya Mpogolo.
Ikumbukwe katika ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi, alizindua Mradi wa Barabara ya Tukuyu Ilala na kuweka jiwe la Msingi katika Sekondari ya Liwiti.