Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM, Dida Shaibu afariki

DAR-Mtangazaji wa Wasafi FM, Khadija Shaibu maarufu kama Dida amefariki leo Oktoba 4,2024 katika Hospitali ya Taifa (Muhimbili) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Wasafi Media. "Uongozi wa Wasafi Media Unasikitika Kutangaza Kifo Cha aliyekua Mtangazaji wa Kipindi Cha Mashamsham cha Wasafi FM Khadija Shaibu (Maarufu kama Dida).

"Dida atakumbukwa kwa Uhodari wake na Ubora wake Kwenye Tasnia ya Habari, Uliompelekea Kuwa Mtangazaji Namba Moja wa Kike Nchini na Kuwa Kioo kwa Wanawake na Watangazaji Wengi waliokua wanamtazama kama Mfano.

"Tunaungana na Ndugu , Jamaa na Marafiki Wote Kusheherekea Maisha Ya DIDA , Na Kuenzi Yale Mengi Mazuri aliyoyafanya Kwenye Jamii na Tasnia ya Uandishi wa Habari .

"Tunamuombea Mungu ailaze Roho yake Mahala Pema Peponi, Amen."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news