DAR-Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma leo Oktoba 10,2024 jijini Dar es Salaam ameonesha rasmi muonekano wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) mbele ya waandishi wa habari.

"Sisi wasaidizi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaona mapenzi ya dhati ya mama yetu kuhusiana na michezo, sanaa na utamaduni wa nchi hii, hivyo hatuwezi kufanya vitu chini ya kiwango, ndio maana tuzo hizi zilikuwa zinaendelea kuhakikiwa," amesema Mhe. Mwinjuma.

"Mwaka huu tumepokea kazi zaidi ya 1440, ikilinganishwa na mwaka jana, katika vipengele 36 vinavyoshindaniwa," aliongeza Dkt. Mapana.
Tags
Habari
Sanaa na Utamaduni
Shirikisho la Muziki Tanzania
Tuzo za Muziki
Tuzo za Muziki Tanzania (TMA)