Naibu Waziri Pinda ajiandikisha katika Mtaa wa Ndemanilwa

NA MUNIR SHEMWETA

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Geophrey Pinda ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiwa katika mstari wakati wa zoezi la kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika mtaa wa Ndemanilwa kata ya Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi tarehe 19 Oktoba 2024.

Mhe. Pinda amejiandikisha Jumamosi katika mtaa wa Ndemanilwa katika kata ya kibaoni halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiajiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika mtaa wa Ndemanilwa kata ya Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi tarehe 19 Oktoba 2024.

Kwa mujibu wa mwandikishaji wa kituo hicho Bw. Dikson Fabian zoezi la uandikishaji katika kituo chake limeenda vizuri na kwa mafanikio makubwa ambapo takriban watu 1,090 wamejitokeza.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiajiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika mtaa wa Ndemanilwa kata ya Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi tarehe 19 Oktoba 2024.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbe Mhe. Geophrey Pinda amesema, kwa kumbukumbu za jimbo lake zinaonesha watu wengi wamejitokeza kujiandikisha.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na wananchi wa kata ya Ndemanilwa mara baada ya kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika mtaa wa Ndemanilwa kata ya Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi tarehe 19 Oktoba 2024.

‘’Nitoe wito kwa watu wote ambao hawajajitokeza kujiandikisha wajitikeze kwa ajili ya kushiriki kuchagua viongozi ambao ni uhitaji wao’’ alisema Mhe. Pinda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news