Naibu Waziri Pinda awataka wananchi kutumia mifumo rasmi kuhifadhi fedha

KATAVI-Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, he. Geophrey Pinda amewataka wananchi kuhifadhi fedha zao katika mifumo rasmi ya kifedha kwa ajili ya usalama.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Islamic Benki cha CRDB Bw. Rashid Rashid alipowasili kata ya Majimoto kuzindua tawi la benki hiyo katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 1 Oktoba 2024.

Mhe. Pinda amesema hayo tarehe 01 Oktoba 2024 katika hafla ya uzinduzi wa tawi la Benki ya CRDB katika kata ya Majimoto iliyopo halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele mkoani Katavi.

"Natambua baadhi yetu tumekuwa tukihifadhi fedha zetu majumbani na hivyo kujiweka katika hatari ya kuzipoteza kutokana na wizi au janga lolote linaloweza kujitokeza," amesema Mhe. Pinda.

Akitolea mfano wa majanga yaliyotokea Manyara wakati wa maporomoko ya matope na mafuriko wilayani Rufiji, amesema katika majanga hayo mawili waliohifadhi pesa ndani waliingia kwenye umasikini ila kwa wale waliohifadhi Benki angalau walikuwa na uhakika wa kuendelea na mipango baada ya kupona madhila yaliyotokana na majanga hayo.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la benki ya CRDB katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 1 Oktoba 2024.

Amebainisha kuwa, uamuzi wa benki ya CRDB kuanzisha tawi katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele ni ishara ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuwajumuisha Watanzania kwenye mfumo rasmi wa huduma za kifedha.

"Ni furaha kubwa kwetu sisi wana Mpimbwe kuona Benki yetu ya kizalendo ya CRDB ikifanyia kazi mahitaji ya wateja wake kwa kusogeza huduma zake karibu zaidi na Watanzania hata waliopo vijijini," amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa kKitengo cha Islamic Banking cha CRDB, Bw. Rashid Rashid amesema, kuanzishwa kwa tawi hilo kutatoa fursa ya mikopo kwa watu wote kwa ile mikopo yenye riba na isiyo na riba kulingana na imani zao.
Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akikata utepe kuzindua tawi la Benki ya CRDB katika kata ya Majimoto iliyopo Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele mkoani Katavi tarehe 1 Oktoba 2024. Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe, Mhe. Silas Ilumba na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Islamic Benki ya CRDB, Bw. Rashid Rashid.

‘’Benki yetu itahakikisha haachwi mtu nyuma kutokana na kigezo chochote yaani ukiweza kufika unapata huduma, hii ni katika jitihada kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma pasipo kukwazika kutokana na imani’’ amesema Rashid.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news