Ni wajibu wetu sote kudumisha amani nchini-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema suala la kuhubiri Amani sio la kuachiwa Viongozi wa dini pekee bali kwa makundi mbalimbali ya kijamii yana wajibu wa kulipa mkazo suala hilo.
Rais Alhaji Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 4,2024 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) na yaliofanyika Msikiti wa Taqwa Bweleo ,Wilaya ya Magharibi B.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa makundi matatu ya kijamii yana nguvu kubwa ya kuhimiza amani ya nchi endapo yatadhamiria kuhubiri amani katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Ameyataja makundi hayo kuwa Wanasiasa, Waandishi wa Habari na Viongozi wa dini na kuyataka kutimiza wajibu wao.
Halikadhalika, Alhaji Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa hakuna jambo litakaloshindikana endapo nchi itakuwa katika Amani,Umoja na Upendo miongoni mwa wananchi. .Akizungumzia maadili amewasisitiza waumini wa Kiislamu kuyaishi maisha ya Mtume Muhammad kwa vitendo kwa kufuata miongozo na maelekezo yake ili kuwa na jamii bora.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news