NIRC yaendelea kutoa elimu Maonesho ya Wiki ya Chakula Duniani Kitaifa mkoani Kagera

KAGERA-Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeshiriki maonesho ya wiki ya chakula duniani ambayo kitaifa yanaendelea mkoani Kagera.
Akifungua maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mkuu wa Wilaya ya Muleba,Dkt.Abel Nyamahanga amesema, Mkoa wa Kagera unakabiliwa na changamoto ya udumavu hivyo amewataka wadau wa lishe wakiwemo washiriki wa maonesho hayo kwa ujumla kushirikiana na serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara y Uendeshaji kutoka NIRC, Salome Njau amesema,tume wamejiandaa kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima kuhusu namna bora ya uzalishaji na majukumu ya tume kama kusimamia,kuratibu na kuendeleza miundombinu yote ya umwagiliaji nchini.
Pia amewataka wakulima mkoani Kagera na maeneo jirani kutumia fursa ya maonesho hayo kujufaika na uwezeshaji unaofanywa na Tume kuhusu kilimo cha umagiliaji lengo ni kuwa na kilimo cha kisasa chenye tija kwa maslahi ya ndani na nje kwa kuilisha dunia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news