NIRC yang'ara maonesho ya Wiki ya Chakula Duniani Kitaifa mkoani Kagera

KAGERA-Naibu Waziri wa Kilimo,Mheshimiwa David Silinde amehitimisha maonesho ya Wiki ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika mkoani Kagera.
Awali ametembelea mabanda ya washiriki wa maonesho hayo likiwemo banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na kusifu hatua zinazochukuliwa katika utekelezaji wa miradi.
Mheshimiwa Silinde amesema, Serikali ina mpango wa kujenga soko la ndizi la kisasa mkoani Kagera ili kuwasaidia wakulima mkoani humo kupata bei nzuri ya mazao yao.
Pia, amewataka washiriki wote wa maonesho hayo kuzingatia mambo waliyojifunza ili kuboresha uzalishaji na hivyo kuwa na uhakika wa chakula na lishe kwa jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Salome Njau amesema kuwa, maonesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwa upande wa NIRC.
Amesema, wameweza kuhudumia wakulima zaidi ya 200 na kutoa elimu ya mbinu bora za kilimo cha umwagiliaji ili waweze kulima kwa ajili ya chakula na biashara kwa ujumla.

Salome ameongeza kuwa, tayari wametangaza tenda kwa ajili ya uchimbaji wa visima vinne ambavyo vitanufaisha Mkoa wa Kagera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news